MMM

MMM: 

SSRA ni nini?

Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA) ilianzishwa chini ya Sura ya 139 ya Sheria ya Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii No. 8 ya mwaka 2008 kama ilivyorekebishwa na Sheria Namba 5 ya mwaka 2012, kwa lengo kuu la kusimamia na Sekta ya Hifadhi ya Jamii. Mamlaka ilianza shughuli zake mwishoni mwa mwaka 2010.

Kwa mjibu wa mamlaka iliyopewa kisheria kama ilivyoelezwa katika Sheria ya Hifadhi ya Jamii, Mamlaka anakabiliwa na jukumu la kusimamia na kudhibiti upatikanaji wa Huduma za Hifadhi ya Jamii nchini

Nini Wajibu Na Majukumu ya SSRA?

Wajibu na Majukumu ya Mamlaka zimeainishwa bayana chini ya Kifungu cha 5(1) cha Sheria ya Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa sekta ya Hifadhi ya Jamii Kazi hizo ni pamoja na :-

i. Kusajili Mifuko, watunzaji na Meneja wa uwekezaji katika sekta ya Hifadhi ya Jamii.
ii. Kudhibiti/kurekebisha na kusimamia utendaji wa Mifuko, watunzaji na Meneja wa uwekezaji
iii. Kuweka mazingira yatakayopanua uwigo wa hifadhi ya Jamii na kuongeza wanachama hasa kwenye sekta isiyo rasmi
iv. Kutoa miongozo ya utendaji sahihi na yenye ubora katika sekta ya Hifadhi ya Jamii.
v. Kutetea na kulinda maslahi ya wanachama
vi. Kuweka mazingira mazuri na yanayofaa kukuza na kuendeleza Sekta ya Hifadhi ya Jamii.
vii. Kumshauri Waziri juu ya Sera na Masuala ya uendeshaji kuhusiana na Sekta ya Hifadhi ya Jamii
viii. Kupanga na kutangaza rasmi miongozo itakayotumika kwa mifuko, watunzaji na wawekezaji
ix. Kusimamia na kupitia upya utendaji wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii
x. Kuanzisha mafunzo, kushauri,kuratibu na kutekeleza mabadiliko ya sheria katika Sekta ya Hifadhi ya Jamii.
xi. Kumteua mtu atakayesimamia Mifuko pale inapobidi
xii. Kurahisisha upanuzi wa wigo wa hifadhi ya jamii kuwafikia wale ambao bado hawajafikiwa ikiwa ni pamoja na makundi/sekta zisizo rasmi.
xiii. Kuendesha mipango ya elimu na uhamasishaji kwa umma juu ya masuala ya hifadhi ya jamii.

Mfumo wa Hifadhi ya Jamii ukoje nchini Tanzania?

Nchini Tanzania mfumo wa Hifadhi ya Jamii umegawanyika katika nguzo tatu (3), kama ifuatavyo;

i. Nguzo ya kwanza- nguzo hii inahusisha Hifadhiya Jamii kwa mfumo wa huduma za kijamii zinazogharamiwa na kodi ya Serikali, mashirika ya wahisani wa ndani na nje na taasisi za kijamii
ii. Nguzo ya pili- katika nguzo hii, Hifadhi ya Jamii inahusisha uchangiaji walazima wa wenye kipato na waliona ajiriwa na ndio nguzo ambayo Mifuko ya Hifadhi ya Jamii inahusika. Uchangiaji katika mifuko hiyo ugharamiwa na Waajiri pamoja na Wafanyakazi.
iii. Nguzo ya tatu- Hifadhi ya Jamii katika nguzo hii hutolewa kwa mfumo uchangiaji wa hiari ambao unawalenga zaidi watu wenye kipato cha ziada na huchangia kama ziada baada ya kutekeleza majukumu ya kisheria kwenye nguzo ya pili.

Je Kuna mifuko mingapi ya Hifadhi ya Jamii Tanzania?

Kuna mifuko sita ya Hifadhi ya jamii Tanzania bara, ambayo ni:
i. Mfuko wa Mafao ya Kustaafu (GEPF )
ii. Mfuko wa Pensheni wa LAPF
iii. Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF)
iv. Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF)
v. Mfuko wa Pensheni wa PPF (PPF)
vi. Mfuko wa Pensheni wa PSPF (PSPF)
Mifuko yote hii inasimamiwa na Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA)

Ni mafao yapi yatolewayo na mifuko ya hifadhi ya jamii?

Kuna aina mbili za mafao yatolewayo na mifuko ya hifadhi za jamii Tanzania, yapo mafao ya muda mfupi na yale ya muda mrefu.

a) Mafao ya Muda mrefu

i. Mafao ya uzeeni
ii. Mafao ya Ulemavu
iii. Mafao ya Urithi

b) Mafao ya Muda Mfupi

i. Huduma za Afya
ii. Kuumia Kazini
iii. Uzazi
iv. Kifo
v. Elimu

Kwanini mafao ya wanachama yamepunguzwa

Mafao hayajapunguzwa bali yameongezwa kwa asilimia 37.5 ambayo pia yalizingatia thamani ya ulipwaji wa pensheni unaendana na gharama za maisha (Indexation). Maboresho hayo yametojana na tathmini za kitaalamu pamoja na maoni ya wadau

Mafao mapya yana anza lini?

Kanuni za Mafao mapya zimeshaanza kutumika rasmu tarehe 01/07/2014, kanuni hizi zimeanza kutumika kwa wanachama wanaostaafu Mfuko a NSSF, PPF na GEPF, hata hivyo kanuni hizi haziwagusi wanachama waliokuwapo PSPF na LAPF kabla ya tarehe 01/07/2014.

Kuna umuhimu gani wa kuwa na Mifuko mingi kwa mafao yamelinganishwa kwa Mifuko yote?

Mwanzoni Mifuko ilianzishwa kisekta. Hata hivyo baada ya kuwianisha mafao, SSRA imepata watathmini Shirika la Kazi duniani (ILO) kufanya tathmini yenye kuangalia namna bora ya kuunganisha Mifuko ikiwa ni pamoja na gharama zitakazojitokeza katika zoezi hilo.

Kwanini Mafao ya Kifo yanacheleweshwa sana?

Mafao ya kifo ucheleweshwa kutokana na uhitaji wa hatua nyingi za uhakiki, SSRA kwa kushirikiana na ILO na Mifuko husika wanalifanyia kazi swala hilo

Je itachukua muda gani mifuko ya PSPF na LAPF kulipa kwa kutumia kikokotoo kipya?

Inakadiriwa kwamba itachukua kati ya miaka 25-35 kwa Mifuko hii kulipa kwa kutumia kikokotoo kipya kwa vile kinaanza na wanachama wapya waliojiunga Julai 1,2014.

Jinsi gani Mifuko ya Pensheni uhusisha Wanachama katika kufanya maamuzi?

Mifuko ya Pensheni uhusisha wanachama na wadau wengine katika kufanya maamuzi kupitia kwa muundo wa Bodi ya Wadhamini linaloshirikisha wadau wa sekta ya hifadhi ya ya jamii katika utungaji wa sera na kufanya maamuzi mengine makubwa kama inavyoelekezwa katika muongozo uendeshaji wa bodi ya wadhamini uliotolewa na mamlaka ya hifadhi ya jamii SSRA
Mkutano Mkuu wa Mwaka ni njia nyingine ya ushiriki muhimu wa wanachama kuhusika katika uendeshaji wa mifuko

Kwa nini Pensheni si kulipa gawio?

Mifuko ya Hifadhi ya Jamii ya lazima Tanzania ni Define Benefits yaani ni mifuko ya pensheni inayofuata misingi ya kibima Mwanachama huahidiwa mafao mbalimbali pamoja na pensheni. Hapa risk ya kuishi muda mrefu pamoja na risk ya uwekezaji hubebwa na mifuko

Umri wa kustaafu nchini Tanzania ni upi?

Kisheria umiri wa kustaafu kwa hiari nchini Tanzania ni miaka 55, na miaka 60 kwa lazima, japokuwa kuna baadhi ya sekta zina umri tofauti wa kustaafu.