Watunzaji wa Mifuko ya Pensheni

Body: 

Mtunzaji katika mifuko wa pensheni ni kampuni ilisajiliwa kisheria ambayo wameajiriwa kwa lengo la kutunza mali ya mifuko ya pensheni. kushikilia na kushughulikia mali kikamlifu  kwa mujibu wa mamlaka na maelekezo aliyopewa kutoka katika Kanuni ya Hifadhi ya  Jamii, ya Mwaka 2009 na Mifuko ya pensheni  yenyewe.

Makampuni haya yamesajiliwa kwa mujibu wa sheria za nchi jukumu kubwa likiwa ni kulinda na kusimamia mali, amana, dhamana, nyaraka za mifuko ya pension

Wajibu na majukumu ya Mtunzaji wa Mfuko wa Pensheni ni pamoja na yafuatayo;

 • Kuhakikisha usalama wa amana na dhamana zinazotenngeneza mali za Mfuko wa Pensheni
 • Kusimama kama wakala wa kupitisha, kununua na kuuza dhamana chini ya maelekezo ya mifuko ya pensheni na kukusanya malipo ya gawio, riba na mapato mengine yote yanayohusiana na uwekezaji wa Mfuko ya Pensheni.
 •  Kupokea michango pensheni kwa niaba ya Mifuko ya Pensheni
 • Kutoa  mahesabu ya Uwekezaji  na taarifa za utendaji.
 • Usimamizi wa majanga na utekelezaji wake. Hii itakuwa ni pamoja na ufuatiliaji wa miongozo ya uwekezaji na  mipaka yake  ilioyoweka na  Sera ya Mifuko ya Pensheni.

Watunzaji Waliosajiliwa Mpaka Sasa

 • CRDB BANK PLC
 •  STANBIC BANK LTD
 • STANDARD CHARTERED BANK LIMITED,
 • BANK M (TANZANIA) LTD
 • AFRICAN BANKING CORPORATION TANZANIA LIMITED
 • AZANIA BANK LIMITED