Mifuko ya Hiari ya Pensheni

Body: 

Mifuko ya hiari(Supplementary Scheme) ilianzishwa kwa Sheria ya Mamlaka ya Usimamizi wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii, Sura ya 135 (Toleo la 2015), lengo likiwa ni kuweka  mpango wa hiari wa wanachama kujichagulia nini cha kuchangia kutoka katika kipato cha ziada baada ya kuchangia kwenye mfuko wa lazima

Kifungu cha 31 cha Sheria ya Mamlaka ya Usimamizi wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii, Sura ya 135 (Toleo la 2015) kinasema kuwa "Mtu yeyote anaweza, chini ya sheria na masharti yaliyowekwa katika Kanuni, kuanzisha mfuko wa ziada ambao uanachama wake atakuwa hiari."

Sheria inatoa pia nafasi ya hii Mifuko ya Pensheni au waajiri kuanzisha iyo mifuko ya hiari. Mifuko hii huruhusu mwanachama kuchukua michango yake yote pale anapoacha kazi au kuhitaji kufanya ivyo, pamoja na kufanya hiyo Mwanachama upewa michango yake yote pamoja na faida kwa kiwango kitakachoamuliwa na mifuko yake.

Mifuko ya Hiari iliyosajiliwa mpaka sasa ni;

 1. Puma Energy Tanzania Provident Fund
 2. Voluntary Savaings Retirement Scheme
 3. MSD Wekeza Supplementary Scheme
 4. Deposit Administration Scheme
 5. PSPF Supplementary Scheme
 6. ELCT Retirement Scheme
 7. Wote Scheme
 8. PPF Staff Supplementary Scheme
 9. BOT Staff Benefits Scheme
 10. TANAPA Group Endowment Fund
 11. LAPF DC Scheme
 12. Tanzania Portland Cement Company Limited Staff Pension Scheme

SSRA inawafahamisha mwanachama wa sasa, mwajiri au mtu yeyote ambaye ana nia kujiwekea akiba kwa ajili ya baadaye kuunda au kujiunga na mifuko hiyo ya hiari

SSRA inapenda kuwafahamisha pia wadau na umma kwa ujumla kwamba inasajili Mifuko ya hiari kwa kufuata Sheria na Kanuni za Hifadhi ya Jamii, 2009.

Wakati huu, Mamlaka hiyo inakaribisha maombi kutoka kwa mtu yeyote ambae anataka kuanzisha Mfuko hiari kuomba usajili kama kanuni na sheria zinavyosema.

Fomu za maombi na kanuni za usajili wa Mifuko ya hiari ya Hifadhi ya Jamii inaweza kupakuliwa kutoka tovuti ya Mamlaka; www.ssra.go.tz.

Nakala halisi zinapatikana makao makuu ya Mamlaka