Watawala

Body: 

Ni Mtu/Kampuni iliyo/alieteuliwa na Bodi ya wadhamini kuendesha shughuli za utawala kwenye Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kulingana na vigezo na matakwa ya huduma ziliainishwa katika makubaliano.

Haya ni makampuni yaliyoanzishwa chini ya Sheria ya Makampuni na kupewa nguvu ya kisheria kimaandishi, hati ya makubaliano au chombo kingine chochote kufanya huduma za kiutawala.

Wajibu na majukumu ya kisheria ya  mtawala yaliyoainishwa kisheria

 • Kufanya shughuli za kiutawala za kila siku za mifuko kulingana na vigezo na matakwa ya huduma zilizoainishwa katika chombo cha uteuzi
 • Kwa kushirikiana  na wadhamini, Mamlaka, inawajibu wa kukusanya kodi za ndani na za watoa huduma kwa utawala wa mfuko,
 • Kutoa huduma za ushauri na mafunzo kwa wadhamini, wanachama juu ya haki  na wajibu wao kwenye Mfuko.
 • Kutoa taarifa Mfuko zinazohitajika kwa watoa huduma ili kuwezesha maandalizi ya marejesho ya kisheria kwa Mamlaka;
 • Kuwasilisha  mrejesho  na taarifa zinazotakiwa kisheria kwa Mamlaka;
 • Kukusanya na kulipa mafao kwa wanachama na wategemezi wao kama ilivyoinishwa kwenye sheria na kanuni za mifuko.
 • Kuandaa bajeti ya mfuko, vigezo vya mzunguko wa fedha na ukwasi kama ikihitajika mara kadhaa.
 • Panapohitajika kutoa huduma za kikatibu kwa bodi ya wadhamini kwa kuandaa mikutano, kutoa taarifa za mikutano hiyo na kuchukua muhutasari katika mikutano hiyo.
 • Kuwashauri wadhamini kuhakikisha kuwa meneja anawekeza fedha za Mfuko kulingana na sheria na kanuni zilizotolewa, bodi ya wadhamini wa Mfuko na nguvu zingine za kisheria zilizopo.

Watawala waliosajiliwa;

 1. PPF Pension Fund
 2. Jubilee Life Insurance Corporation of Tanzania Ltd