Mifuko ya Bima ya Afya

Body: 

Kwa nia njema ya  kuhakikisha huduma za afya bora na nafuu kwa wafanyakazi wa umma, mashirika binafsi na makundi mengine, zinapatikana kwa wanachama wachangiaji na wategemezi wao. Serikali iliangalia njia mbadala kwa kuanzisha mfuko wa huduma za afya ilikutekeleza Mageuzi ya Sera ya Sekta ya Afya (1993/3). Matokeo yake mwaka 1999 serikali ilianzisha  Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya kama Taasisi ya Umma chini ya Sheria Na.8 ya 1999 (sura ya 395, kama ilivyorekebishwa Mwaka 2002)

Uchangiaji

Mfuko huu una mfumo wa uchangiaji, na kiwango ambacho mtu huchangia kwa kiasi kikubwa inategemea uwezo wa kulipa na si kiwango cha hatari kinachoweza kujitokeza, jinsia au kiwango cha matumizi ya awali   ya mwanachama au wanachama wanaotazamiwa.

 Kwa mujibu wa Sheria NHIF, waajiri na wafanyakazi katika sekta ya umma ni wajibu wao kujiandikisha  na kuchangia katika Mfuko jumla asilimia sita  ya mshahara mwezi wa kila mfanyakazi  ambayo huchangiwa kwa pamoja kati ya mwajiri na mwajiriwa. Mfuko umeweka bayana utaratibu wa uchangiaji kwa makundi mengine maalumu kama vile wanafunzi, viongozi wa dini, vyama na watu binafsi kusajiliwa na Mfuko

Walengwa

Mfumo huu unazingatia muundo wa maisha ya Kiafrika  ya kutunza watoto na wazazi wa wachangiaji. Wanafaika wa NHIF ni pamoja na mwanachama mchangiaji, mke na hadi wategemezi wanne ambao wanatambulika kisheria. Kwa mazingira ya NHIF, wategemezi ni pamoja na watoto wa damu au watoto waliorithiwa kisheria na wazazi.

Mfuko wa Afya ya Jamii

Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF) ni Mfuko wa hiari ulioanzishwa na Sheria No 1 ya 2001. Mfuko ulianzishwa kwa mara ya kwanza nchini kama majaribio mwaka 1996, Wilayani Igunga. CHF ni mfuko ulioundwa katika ngazi ya halmashauri kwa mfumo wa malipo ya kabla ukiwa na lengo la kuwezesha jamii kupata huduma za afya kwa gharama nafuu ambazo zitaamuliwa na jamii husika.