Mfuko wa hiari huanzishwa na kampuni au taasisi kwa lengo la kutoa mafao au huduma zingine ambazo haizitolewi na Mifuko ya lazima. Aidha, wanachama wake watakuwa na uwezo wa kujichagulia kiwango cha kuchangia katika Mfuko huu baada ya kuchangia kwenye mfuko wa lazima

Kifungu cha 31 cha Sheria ya Mamlaka ya Usimamizi wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii, Sura ya 135 (Toleo la 2015) kinasema kuwa "Mtu yeyote anaweza, chini ya sheria na masharti yaliyowekwa katika Kanuni, kuanzisha mfuko wa hiari ambao uanachama wake utakuwa hiari."

Mifuko ya Hiari iliyosajiliwa na Mamlaka ni;

 1. Puma Energy Tanzania Provident Fund
 2. Voluntary Savings Retirement Scheme
 3. MSD Wekeza Supplementary Scheme
 4. PSPF Supplementary Scheme
 5. ELCT Retirement Scheme
 6. Wote Scheme
 7. PPF Staff Supplementary Scheme
 8. BOT Staff Benefits Scheme
 9. TANAPA Group Endowment Fund
 10. LAPF DC Scheme
 11. Tanzania Portland Cement Company Limited Staff Pension Scheme
 12. Deposit Administration Scheme
 13. Tumaini Pension Fund
 14. National Informal Sector Scheme
Go to top