Mifuko ya Pensheni

Hifadhi ya Jamii ni mfumo ambao jamii husika hujiwekea kwa lengo la kujikinga dhidi ya majanga yasiyotarajiwa. Majanga hayo ni kama Maradhi, Ulemavu, Kupoteza kazi, Kuacha kazi kwa sababu ya uzee (kustaafu).

Sera ya Mifuko ya Hifadhi ya Jamii

Nchini Tanzania mfumo wa Hifadhi ya Jamii umegawanyika katika nguzo kuu tatu (3), ambazo ni:

 • Nguzo ya kwanza - Nguzo hii inahusisha Hifadhi ya Jamii katika mfumo wa huduma za kijamii zinazogharamiwa kwa kodi ya  Serikali, mashirika ya wahisani wa ndani na nje na taasisi za kijamii
 • Nguzo ya pili - Katika nguzo hii, Hifadhi ya Jamii inahusisha uchangiaji wa lazima kwa wenye kipato na walio katika ajira. Hii ndio nguzo ambayo Mifuko ya Hifadhi ya Jamii inahusika. Uchangiaji katika mifuko hiyo ugharamiwa kwa pamoja kati ya Waajiri pamoja na Wafanyakazi.
 • Nguzo ya tatu - Hifadhi ya Jamii katika nguzo hii hutolewa kwa mfumo uchangiaji wa hiari ambao unawalenga zaidi watu wenye kipato cha ziada na huchangia kama ziada baada ya kutekeleza majukumu ya kisheria kwenye nguzo ya pili.

Mfuko wa Pensheni

Mfuko wa pensheni ni uwekezaji wa mali unaolenga kuzalishaji na  ukuaji wa uchumi imara kwa muda mrefu, na kutoa pensheni kwa wafanyakazi pindi watakapofika ukomo wa kufanya kazi  na kuanza maisha ya kustaafu.

Mifuko ya Pensheni Nchini Tanzania

Tanzania Bara kuna Mifuko ya pension ya lazima miwili nayo ni;

 • Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF)
 • Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF)

Kwa ujumla Mfuko hii yote husajiliwa na kusimamiwa na Mamlaka ya Usimamizi na udhibiti wa sekta ya hifadhi ya jamii

Umuhimu wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii.

 • Kuongeza wigo wa Hifadhi ya Jamii (Social Security Coverage)
 • Kupunguza umasikini kwa Watanzania
 • Kuongeza kinga kwa Watanzania katika Nyanja kama vile elimu, afya, uzazi, ulemavu na uzee.
 • Kuongeza uwekezaji na kutoa fursa kwa Wajasiriamali kupitia vikundi mbalimbali vya kijamii
 • Kuchangia maendeleo ya miradi mbalimbali ya Serikali
 • Kuongeza ajira kwa Watanzania kupitia miradi inayoendeshwa na Mifuko hiyo

Mafao yanayotolewa

Kuna aina mbili za mafao yatolewayo na mifuko ya hifadhi za jamii Tanzania;  mafao ya muda mrefu na muda mfupi

Mafao ya Muda Mrefu

 • Pensheni ya Uzeeni - kustaafu
 • Pensheni ya Ulemavu
 • Pensheni ya Urithi (kifo)

Mafao ya Muda mfupi

 • Uzazi – kwa baadhi ya mifuko
 • Kuumia kazini – kwa baadhi ya mifuko
 • Afya – kwa baadhi ya mifuko
 • Msaada wa mazishi
 • Elimu – mfuko mmoja

Uhusika wa sekta isiyo rasmi kwenye Mifuko ya hifadhi ya Jamii

Sekta isiyo rasmi inahusika katika Mifuko isiyo rasmi kwa kujiunga kwenye mfumo wa huchangiaji wa hiyari unaratibiwa na Mifuko ya pensheni.lakini pia sheria inawapa uhuru wa kuanzisha mifuko ya hiari kwenye sehemu au makundi yao ya kazi na kuisaji kwa mamlaka.

 

 

Go to top