Kwa nia njema ya  kuhakikisha huduma za afya bora na nafuu kwa wafanyakazi wa umma, mashirika binafsi na makundi mengine zinapatikana kwa wanachama wachangiaji na wategemezi wao, serikali ilianzisha  Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya kama Taasisi ya Umma chini ya Sheria Na.8 ya 1999, Sura ya 395, [Kama Ilivyofanyiwa Marekebisho].

Uchangiaji

Kwa mujibu wa Sheria NHIF, waajiri na wafanyakazi katika sekta ya umma wana wajibu wa kujiandikisha  na kuchangia katika Mfuko jumla ya asilimia sita  ya mshahara wa mwezi wa kila mfanyakazi   ambapo kiwango hiki huchangiwa kwa pamoja kati ya mwajiri na mwajiriwa. Mfuko umeweka bayana utaratibu wa uchangiaji kwa makundi mengine maalumu kama vile wanafunzi, viongozi wa dini, vyama na watu binafsi kusajiliwa na Mfuko

Walengwa

Wanuafaika wa NHIF ni mwanachama mchangiaji, pamoja na wategemezi wanaotambulika kwa mujibu wa sheria.

Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF)

Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF) ni Mfuko wa hiari ulioanzishwa na Sheria ya Bunge Na 1 ya Mwaka 2001. Mfuko huu ulianzishwa kwa lengo la kupanua huduma za afya kwa idadi kubwa ya wafanyakazi wasio katika sekta rasmi nchini Tanzania na idadi kubwa ya watu wanaoishi maeneo ya vijijini katika kiwango nafuu cha uchangiaji ambacho huamuliwa na wanajamii wenyewe.

Hadi sasa, jumla ya CHF 164 zimesha sajiliwa na Mamlaka ya Hifadhi ya Jamii.

 

Go to top