Tamko hili linahusu SSRA, mtu mwingine yeyote, chombo kilichotambuliwa kisheria kinachodhibiti, kudhibitisha au kutumia taarifa zinazopatikana na kupitia tovuti hii.Mtumiaji anaweza kutembelea tovuti hii bila kutoa taarifa zake. Hata hivyo mtumiaji anaridhia matumizi ya taarifa hizo kwa mujibu wa tamko hili.

 

Taarifa zinazokusanywa

Taarifa binafsi ambazo zitakusanywa  na SSRA zitatumiwa na kuwekwa wazi na SSRA tu.

 Wakati unatembelea tovuti ya SSRA tunaweza kuhifadhi baadhi ya taarifa ikiwa ni pamoja na: anwani ya mtandao ambayo ulitumia kuingia kwenye Tovuti ya SSRA, tarehe na muda, anwani ya tovuti ambayo uliunganishwa na Tovuti ya SSRA, jina la maneno na faili uliyotafuta, vitu vilivyoguswa kwenye ukurasa. Taarifa zitakazokusanywa zitatumika kubaini idadi ya wageni waliotembelea sehemu mbalimbali ya tovuti yetu na kutambua maeneo ya tatizo. SSRA pia itatumia taarifa hii ili kuboresha na kufanya tovuti iwe muhimu zaidi.

 

Taarifa binafsi

Taarifa binafsi hazitakusanywa kwa matumizi yoyote yale isipokuwa kwa ajili ya  kujibu maombi yako. Taarifa zilizopo kwenye fomu ya kujaza  malalamiko na mapendekezo zitakuwa kwa matumizi ya kujibu ujumbe wako na kukusaidia kupata taarifa ulizoomba.

 

Jinsi ya Kuwasiliana Nasi kuhusu Tovuti

Kama una swali lolote kuhusu namna  taarifa yako  ilivyotumika  katika uhusiano na tovuti hii au kuhusu SSRA sera ya faragha na mwenendo wa taarifa , unaweza kuwasiliana nasi kwa kutumia kiunganishi cha malalamiko / mapendekezo iliyopo katika  tovuti hii au kiunganishi cha  "maoni" au kwa kututumia kwa barua pepe : Anwani ya barua pepe hii inalindwa kutokana na spambots. JavaScript lazima iwe itawezeshwa kwa kuweza kuona.

Tafadhali kumbuka: Tovuti hii inaweza kuwa na viunganishi vya tovuti zingine ambazo hazilindwi na kauli hii ya  faragha.

Go to top