MMM

  1. Je, makampuni ambayo Serikali inamiliki asilimia 30, hisa hizi zikipungua wafanyakazi wa makampuni haya ambao ni wanachama PSSSF bado watakua na sifa za uanachama kwenye Mfuko huu?

Kanuni ya 55 ya Kanuni za jumla za Mfuko wa PSSSF zimelekeza kuwa wafanyakazi wa makampuni ambayo Serikali inamiliki asilimia 30, hisa hizi zikipungua wafanyakazi wa makampuni haya bado wataendelea kuwa wanachama wa PSSSF mpaka hapo Waziri mwenye dhamana ya Hifadhi ya Jamii atapo elekeza vinginevyo.

2.  Je, kigezo gani kilitumika kuamua kuwa wafanyakazi watakao ajiriwa katika makampuni ambapo Serikali ina hisa asilimia 30 wawe wanachama wa Mfuko wa PSSSF?

 Uamuzi wa kutumia kiwango cha umiliki wa hisa wa asilimi 30 kilizingatia  idadi ya makampuni husika kwa mujibu wa Orodha ya Makampuni ambako Serikali ina hisa kutoka kwa Msajili wa Hazina

3.  Je, wafanyakazi waliokuwa wameandikishwa kwenye Mifuko inayounganishwa wataandikishwa tena?

 Hapana wanachama wa Mifuko iliyounganishwa hawato andikishwa upya. Kanuni ya 5 ya Kanuni za Jumla za Mfuko wa PSSSF imeeleza kuwa baada ya miezi 6 ya Mfuko wa PSSSF kuanza shughuli zake wanachama wote wa Mifuko iliyounganishwa watapatiwa vitambulisho vipya.

4.  Je, wafanyakazi wa sekta ya umma waliopo NSSF na wa sekta binafsi waliopo PSSSF, watahamishwa kwenda kwenye Mifuko ya sekta husika?

Hapana, kifungu cha 5 cha Sheria Na. 2 ya Mfuko wa PSSSF kimeeleza kuwa kuanzia tarehe ya kuanza kutumika sheria Na.2 wanachama wote wa Mifuko iliyounganishwa watakua wanachama wa PSSSF bila kujali sekta ya ajira. Vivyo hivyo, kwa wanachama wa sekta ya umma waliopo kwenye Mfuko wa NSSF wataendelea kuwa wanachama wa Mfuko huo mpaka watakapo amua kubadili sekta ya ajira. Isipokuwa usajili wa wanachama watakaoajiriwa kuanzia tarehe 01/08/2018 utazingatia sekta ya walizo ajiriwa

5.  Je, utaratibu wa kuchangia asilimia 15 kwa 5 kwa Mfuko wa PSSSF utazingatiwa pia kwenye Mfuko wa NSSF ambapo mwanachama hulazimika kuchangia asilimia 10?

Mabadiliko yaliyofanywa kwenye Sheria ya NSSF kupitia sheria Na.2 ya Mwaka 2018, yamebadilisha muundo wa namna ya uchangiaji, ambapo imeweka utaratibu ambao kwa kuzingatia majadiliano na makubaliano baina ya mwajiri na mfanyakazi unuruhusu kubadilisha viwango hivyo vya uchangiaji isipokuwa katika makubaliano hayo mwanachama hapaswi kuchangia zaidi ya nusu ya kiwango cha uchangiaji kwa mwezi.

Tovuti Muhimu